Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-xq6d9 Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:08:15.774Z Has data issue: false hasContentIssue false

34 - Wakati Wa Uwanafunzi

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Wakati wa furaha kubwa kabisa

  • 2. Hapana wasiwasi

  • 3. Ni msingi bora wa wakati wetu ujao

  • 4. Kazi na madaraka ya wakati wa uwanafunzi

Kama watu wote walioelimika wangeulizwa mmoja mmoja, “Wakati gani wa furaha kubwa kabisa wa maisha yako?” jibu lingekuwa kwamba wakati wa muda wa uwanafunzi ni wakati wao wa furaha kubwa kabisa katika maisha yao. Labda wanafunzi walio katika wakati huo hasa wasingekubali; lakini hawajui furaha zake zilivyo mpaka wameona hakika halisi za maisha ya baadaye. Wakati wamepata mapigo na misiba mizito ya maisha ndipo watazamapo nyuma wakasema tu, “A! Nilikuwa na furaha iliyoje nilipokuwa kijana! Lakini siku njema za zamani hazitanijia tena!” Tazama kweli iliyo katika methali, “Msifu mvua imempiga.”

Mtu hana udhia wala wasiwasi wa kujua nyumba ikimiwavyo, chakula alacho na nguo avaazo zijavyo. Mtu hana wasiwasi ila hufurahia vitabu, michezo, marafiki zake wa skuli, na safari zake za kila kipindi. Ni kweli kwamba mwanafunzi ana mashaka yake pia, hasa wakati upanga wa mtihani uning’iniapo juu ya kichwa chake, lakini mashaka haya ni madogo sana yalinganishwapo na mashindano magumu ya maisha ambayo lazima tupambane nayo kwa kicheko.

Wakati ikubaliwapo kwamba wakati wa uwanafunzi ni wakati wa furaha kubwa kabisa katika maisha yetu, isingesahauliwa kwamba ni wakati vile vile wa kujiandaa na wakati wa kuweka msingi wa maisha ya wakati ujao. Kama methali isemavyo, “Udongo upate ungali maji.” Mtu hufunzwa katika utoto wake. Mbegu ikipandwa, yote yabakiayo ni wakati wa kuchanua na kuvuna. Tukiwa wakuu au wadogo, waadilifu au wapotofu, waelekevu au washupavu, waaminifu au wadanganyifu, wema au wabaya hutegemea kabisa juu ya mafundisho yetu ya wakati wa uwanafunzi. Kama tumedharau au tumeharibu wakati wetu wa uwanafunzi, hapana la kubakia ila kujuta mwishoni.

Kwa hivi jambo bora ni kwamba wakati huu wa maisha yetu ungetumiwa kwa busara. Wakati wa uwanafunzi usionekane kama wakati wa furaha na raha tupu. Una kazi na madaraka yake. Kazi ya kwanza ya mwanafunzi ni kuwa mtii. Mwanafunzi ni kijana, hana hatia naye mjinga. Akili zake za kujifikiria mwenyewe hazijakua. Hajui jema wala baya kwake. Kwa hiyo wajibu wake ni kutii walimu au walezi wake wanaomtakia usitawi. Utii hutukuza mtu. Watawala wakubwa kabisa wa dunia ni watumishi watii kabisa wakati huo huo. Utii peke yake ndiyo uhalalishao mtu kutawala.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 65 - 67
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×