1. Kitabu ni rafiki, mwalimu na mwongozi
2. Uchaguzi na uangalifu wa vitabu
3. Vitabu vya mafundisho na mazungumzo
4. Maongozi ya vitabu vizuri na vibaya
5. Maendeleo ya elimu baada ya masomo ya kawaida
Vitabu vimehifadhi, kila tunu na hedaya,
Ndiyo hazina kabidhi, ya mambo ya dunia,
Soma upate hadhi, uwe ndege wa kupaa,
Ufunguo wa ardhi, ni kuelewa kitabu.
Vitabu ni marafiki kwa wanadamu. Viko chini ya amri yao siku zote. Ukurasa wa kitabu kilichopigwa chapa ni usemi bora usiotoweka. Haupingwi na wakati wala nafasi. Huwapa mafundisho na faida kubwa watu walionavyo. Vitabu ni hazina bora kuliko hazina ya mfalme yeyote. Ni machimbo azizi ya usanifu, maandiko, ujuzi na maarifa. Mashaka si kusoma, ila ni kusoma nini. Kitabu kizuri ni rafiki, mwalimu na mwongozi kwa watu.
Iliwapasa babu zetu kwenda safari kubwa kusikiliza maneno ya mtu mwenye hekima. Sasa hekima imo kati ka vitabu mezani petu inatungoja. Kwa kweli, kuna vitabu vingi sana. Husemwa kwamba kuna vitabu vya kitambo, tusomavyo kwa kitambo kisha tukavitupa. Kuna vitabu vya nyakati zote, tupendavyo kusoma mara kwa mara, kama mpenzi asomavyo mara kwa mara barua ya kipenzi chake. Hivyo, katika wakati huu uliojaa vitabu vizuri na vibaya, uchaguzi wa vitabu ni mashaka makubwa. Tusiharibu wakati wetu ujao kwa kitabu chochote hafifu, ambacho sifa yake kubwa ni jina zuri na jalada la kupendeza tu. “Nyumba nzuri si mlango, fungua uingie ndani” ni methali ya mwongozo mkubwa katika uchaguzi wa vitabu.
Imesemwa kwamba vitabu fulani vimepasa kujaribiwa yaani, tupekue kurasa zake na tutazame yaliyomo; baadhi yake lazima vimezwe, yaani, visomwe vyote toka jalada hata jalada; na vingine vichache vimebidi kutafunwa na kuyeyushwa, yaani, visomwe mara kwa mara. Ni bora kusoma kwa kujifundisha kuliko kwa kujizungumza, ingawa kusoma kwa kujizungumza kuna manufaa yake, hasa kwa mtu mwenye kazi ngumu. Kuna vitabu bora vya zamani na vya sasa vya kusoma vile vile. Visomwe vipi? Rai iliyotolewa ni kwamba kwa ujuzi, lazima tusome vitabu vipya kabisa; kwa maandiko, vitabu vya zamani kabisa.
Vitabu vibaya vikiingia mikononi mwa vijana, akili zao huambukizwa na maongozi yake maovu. Vijana wengi hodari wameangamia, kwa sababu ya kusoma vitabu vibaya. Vitabu vizuri hutakasa. Hukaza tena husitawisha akili vikajenga na tabia yetu. Kwa matumizi ya vitabu mbalimbali Bacon atushauri kwamba historia hutia busara, mashairi huleta akili, na hesabu huongeza werevu. Lakini kila mtu akubali kwamba kusoma husitawisha mtu.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.