Published online by Cambridge University Press: 17 April 2025
1. Utajiri hushawishi mno
2. Manufaa ya utajiri
3. Tamaa ya umashuhuri bora
4. Umashuhuri kwa utajiri
5. Manufaa ya umashuhuri
Mtu akianza maisha yake katika dunia, huvutwa na masharti mawili, yaani utajiri au umashuhuri. Yapasa kufanya kusudi lake juu ya jambo moja katika mambo haya mawili, maana kupata yote mawili ni vigumu sana, huenda isiwezekane.
Mwanzo wa kufikiri tu, twaona utajiri hushawishi mno. Waswahili husema, “Fedha huvunja nguu na milima ikalala.” Fedha hutupa njia za kupata tutakacho. Twaweza kula chakula kizuri, kuvaa nguo nakawa, kukaa katika majengo ya fahari, kufanya karamu bora, kuzuru nchi ngeni, tukawa na anasa nyingine nyingi kwa msaada wa utajiri. Tukiwa na fedha twaweza kusaidia ndugu na marafiki zetu katika shida. Hivyo fedha hutupa kila kitu tutakacho.
Kwa hali kama hii, umashuhuri hushindwa na utajiri. Umashuhuri hauwezi kutupatia chochote katika vitu hivi. Twaona mara kwa mara watu mashuhuri katika dhiki za fedha.
Tamaa ya utajiri hutufanya hodari. Mtaalamu amesema kweli kwamba maendeleo yetu ya sasa katika hali zote za maisha ni matokeo ya tamaa ya utajiri. Tamaa ya umashuhuri mtupu ya wachache katika sisi ingetutia gizani.
Ni mamoja kabisa tamaa ya umashuhuri ni bora kuliko tamaa ya fedha. Katika kuchuma au hasa kukusanya fedha, twatumia mara kwa mara njia za unafiki. Yatupasa kurairai fulani, kumpa rushwa fulani na kumdanganya fulani. Kwa desturi haiwi hivi katika kupata umashuhuri. Mshairi au msanifu hawezi kupata umashuhuri kwa njia za unafiki. Lakini katika mambo ya siasa, watu wengine hutumia hila ili wapate umashuhuri.
Utajiri hututia katika maovu mengi, lakini umashuhuri hausaidii maovu. Hili halisemi kwamba watu mashuhuri hawana maovu. Lakini yawapasa kuepukana na maovu ili wadumishe umashuhuri wao. Utajiri mzito, lakini umashuhuri mwepesi kama unyoya.
Mtu akichunuka utajiri ana choyo kikubwa. Hutaka utajiri kwa takua. Tumesikia mifano ya watu wengi waliohini nchi zao kwa sababu ya fedha. Watu mashuhuri huweza kuwa na choyo cha namna fulani, lakini hujua kwamba umashuhuri wao umetegemea sifa zao, kwa hivyo huwapasa kujiweka katika mwendo fulani. Uhaini wao wa nchi zao utabadili mara moja umashuhuri wao kuwa ukorofi. Utajiri hauleti umashuhuri kwa tajiri, ingawa kwa kupendekeza twasema ana sifa nyingi za akili na wema.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.