Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-2z2hb Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:28:21.513Z Has data issue: false hasContentIssue false

23 - Twaishi Kwa Matendo Si Kwa Miaka

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Maana

  • 2. Tofauti kati ya maisha na uhai

  • 3. Kusudi la maisha

  • 4. Uzuri au utukufu wa maisha hauhusiani na miaka

  • 5. Umri mrefu usio na matukio na maisha haba yenye matukio

  • 6. Waridi na sifa yake

Maneno haya ya akili ni matokeo ya maarifa na busara nyingi ya mtaalamu mkubwa wa Kizungu. Hapana shaka Wazungu wanakwenda katika njia ya maisha yenye nuru pande zote.

Tuelewapo maana yake yote, twaona kwamba hii ni kweli moja katika kweli kubwa za maisha. Maisha ni nini? Ni kuishi na kumea kama mti? Au, ni kuchanua kama ua? Swali letu ni kwamba, maisha huhesabiwa kwa miaka au kwa matendo? Jawabu ni kwamba maisha huhesabiwa bora au duni kwa sababu ya ubora au uduni wa matendo, si kwa kuhesabu miaka yetu tu. Tukihesabu maisha kwa wingi wa miaka tuishio, mzee wa miaka zaidi ya mia moja aweza kuitwa mtu bora sana kati yetu, na kijana mwenye matendo mengi mema hana cheo cha ubora hata kidogo.

Lakini pana mwanya wa tofauti kati ya maisha na uhai. Uhai ni kukua kwa miaka tu, sawa kabisa na mti umeavyo mwaka kwa mwaka, na kama nyasi ziotavyo kondeni. Maisha yasiyo azimio, tamaa au matendo mema ni uhai tu; walakini, maisha yenye maazimio na tamaa bora, yaliyojaa matendo na matukio, yenye maendeleo na bidii nyingi, ndiyo maisha ya kweli. Maisha haya ya kweli hayahesabiwi kwa wingi wa miaka tu, lakini kwa matendo makuu, ya akili na faida tuletayo. Mtu kama huyo huweza kuishi muda wa miaka thelathini lakini ndiye simba. Utaona wanaume na wanawake wazee wamepindukia umri wa ajabu wa miaka mia moja lakini si wanaume na wanawake kama Muyaka, Mkwawa, Mwaketa na Mwana Kupona walivyokuwa. Kwa nini sivyo? Kwa sababu, hatupimi ubora au utukufu wa maisha kwa miaka ila kwa matendo.

Uzuri au utukufu wa maisha hauhusiani na miaka. Upindi wa mvua mzuri huonekana kwa muda wa dakika chache mbinguni, lakini huishi sana mioyoni mwetu baada ya kutoweka mbinguni. Twahesabu mti kuwa na manufaa, si kwa wingi wa majani yake lakini kwa matunda uzaayo. Vivi hivi, twahesabu ubora au uduni wa maisha yetu kwa matendo mema na matukio bora katika wakati wetu.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 46 - 48
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×