1. Maendeleo yote huja kwa tamaa
2. Hatari ya tamaa ya choyo
3. Tamaa hutukuza mtu, nchi na taifa
4. Tamaa kati ya wakuu na wadogo
5. Maovu ya tamaa mbaya
6. Tamaa ni mbaya au nzuri kwa matumizi yake
“Tamaa jambo muhimu kuwa nalo duniani.” Dunia isingeendelea hata kidogo kama pasingekuwa na tamaa. Maendeleo yote huja kwa tamaa. Dunia hivi ilivyo, ni matokeo ya tamaa; dunia itavyokuwa, ni mazao ya tamaa vile vile. Tamaa ni uwezo mkubwa ulio nyuma ya matendo na mawazo ya wanadamu.
Tamaa yaweza kutufaidia sisi wenyewe, kusitawisha nchi na kufadhili taifa. Lakini tamaa ya maazimio ya choyo na ile ionekanayo ina udanganyifu na njia mbaya ni tamaa ya aibu. Ina hatari kubwa kabisa iwapo imeng’ang’aniwa na watu wenye nguvu au uwezo. Kwa tamaa ya wazimu wa kushinda dunia, kwa sababu ya kuridhisha furaha ya uwezo, watu wamepigana bure wakauana makusudi.
Pengine tamaa ikiongozwa vema, huwa sababu ya heri kubwa kwa watu. Tamaa kama hiyo huendesha gurudumu la maendeleo daima. Ni msingi wa magunduzi na mavumbuzi yote bora. Magunduzi ya ujuzi, na vipeo vya elimu kubwa za dunia, hutokana na tamaa bora za wasanifu za kutenda neno ambalo dunia haitakubali lipotee. Kazi kama hizo hufanywa kwa nia ya kufadhili walimwengu. Sifa na heshima wapatazo watu kama hao hufuata tu.
Tamaa haionekani kwa wakuu tu, lakini hata kwa watu wadogo kabisa. Kila mtoto wa skuli ana tamaa ya kuwa mtoto bora kabisa. Karani ana tamaa ya kuwa karani mkubwa. Mwalimu wa skuli ana tamaa ya kuwa mwalimu mkuu. Katika kila njia ya maisha twakutana na tamaa. Ni adimu kuona mtu ambaye hana tamaa ya namna fulani.
Yaaminika kwamba tamaa njema hutupeleka katika tamaa bora, lakini tamaa ya aibu, ambayo haifaulu, hugeuka uovu, wivu, ushindani na ujinga. Mtu mwenye tamaa mbaya hufanya neno lolote na ujasiri wowote. Hata kwa ajili ya tamaa bora lazima pawe na mpaka, maana, tamaa isiyo mpaka hupoteza mtu. Tamaa isiyo choyo huleta heri; tamaa ya choyo na aibu ni laana. Ni dhahiri kwamba tamaa ni sawa na upanga uwezekanao kutumiwa kwa kazi njema au mbaya; na tamaa ni njema au mbaya kwa sababu ya matumizi yake tutumiayo.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.