Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-twqc4 Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T06:58:31.374Z Has data issue: false hasContentIssue false

33 - Shida Ya Chakula

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Sababu zake

  • 2. Dhiki ya watu

  • 3. Dhiki ya wanyama

  • 4. Shida ya maji

  • 5. Shida ya chakula zamani na sasa

  • 6. Kazi ya faraja

Nchi ya ukulima kama Afrika Mashariki hutaabishwa na njaa mara kwa mara. Hili hutokea mazao yasipopatikana kwa sababu ya nzige na shida ya mvua. Nzige ni wadudu waharibifu sana kwa mimea. Mvua za kutangulia kabla ya wakati, zile za kuchelewa, kuuza mavuno yote na ukulima mdogo ni sababu nyingine ziongozazo sehemu nyingi za nchi hii katika njaa.

Mazao yasipopatikana, matajiri huficha vyakula, kwa hiyo bei zake hupanda. Watu maskini hawawezi kununua chakula kwa bei kubwa na kwa hiyo lazima wapunguze mahitaji yao.

Hali ya chakula huzidi kuwa mbaya kidogodogo. Njaa huenea pande zote, hutia ukiwa katika nchi ikakatisha watu tamaa. Wanawake na watoto wengi hulilia chakula, lakini hapana chakula cha kuwaokoa. Mwisho wengi wao hufa kwa njaa. Watu wengi hula majani na mizizi ya miti. Hata vitu hivi huadimika pia. Wengine hutafuta chakula katika majaa. Watu huenda huku na huko, hawaoni mtu hata mmoja wa kuwakaribisha ila njaa. Kwa hali hii watu hulilia chakula na mwisho wao wenyewe huwa chakula cha njaa.

Dhiki ya wanyama kama ng’ombe, kondoo, na mbuzi huzidi kuwa mbaya wakati misitu ya malisho ionekanapo kama jangwa. Hutangatanga huku na huko wakilia kutafuta takataka yoyote waonayo njiani. Kwa muda mdogo nchi hutapakaa magofu ya wanyama. Fikiri Wamasai ambao huishi kwa maziwa na nyama. Hali yao huwaje wakati huo.

Shida ya maji huzidisha hali kuwa mbaya mara kwa mara. Visima, maziwa na mito mingi hukauka. Wanadamu na wanyama hudhuriwa sana na kiu. Jitihadi hufanywa za kuleta maji toka nchi za karibu, lakini hayatoshi. Hapo hali ya wanyama huzidi kuwa mbaya pia.

Kwa desturi njaa hufuatana na majinai na maambukizo. Watu hufanya namna zote za majinai ili wapate chakula. Mapokeo ya watu wa Afrika husema kwamba njaa ilisaidia nusu ya biashara ya utumwa. Tena shida za chakula na maji huleta maambukizo kama kipindupindu, kuhara damu na kadha wa kadha.

Kwa kweli sasa njaa haina dhara kubwa kama ilivyokuwa zamani. Twashukuru majilio ya motakaa, reli, meli na eropleni maana chakula huwezekana kupelekwa upesi katika nchi zenye njaa.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 63 - 65
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×