Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-2z2hb Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T10:17:00.662Z Has data issue: false hasContentIssue false

47 - Nchi Ambayo Ningependa Sana Kuzuru

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Uingereza imeniingia sana moyoni

  • 2. Utukufu wake washawishi

  • 3. Ushawashi wa miji na mashamba

  • 4. Viwanda na majahabu

  • 5. Watu wa Uingereza

“Safari ni hatua” ndiyo kusema safari ni majaliwa. Endapo nikipata hatua ya kusafiri nataka kuzuru nchi za mabara makuu yote. Lakini katika nchi hizo zote moyo wangu umeshawishika sana kuzuru Uingereza.

Uingereza imeniingia sana moyoni kwa sababu nafikiri ni johari ya Ardhi. Ilinganishwapo na mabara makuu ya ulimwengu ni kisiwa kidogo kama nyota ilinganishwapo na jua au mwezi mbinguni, lakini utukufu wake mkubwa kabisa. Nataka kuona nchi hii ilivyofikia kilele cha utukufu wa ulimwengu.

Uingereza ni nchi ya busara na jitihadi. Ina mwenge mkononi mwake wa nuru ya uongozi. Matendo yake makubwa na ya kuajabiwa yanishawishi sana kuizuru. Nina hamu kubwa ya kuona watu wa Uingereza waishivyo na wafurahivyo.

Nataka kuona mambo na mahali kadha wa kadha huko Uingereza. Kwanza nitatazama Halmashauri Kuu zilizo London. Ushawashi wangu wa pili ni kutazama vyuo vya Oxford na Cambridge; maktaba mashuhuri ya Makumbusho ya Kiingereza; Thames, malkia wa mito ya ulimwengu na bandari yake; na mambo mengine matukufu. Nitatumia nafasi vile vile ya kuwa abiria katika magari ya moshi ya chini ya ardhi.

Tena nitashika njia mpaka Edinburgh kazi zangu zilikopigwa chapa. Huko ni Scotland. Nitapanda milimani niburudishe katika mwili wangu joto la jua la Afrika. Baadaye nitatembea makondeni kutazama ukulima mpya na mazao yake.

Kisha nitafika Ireland alikozaliwa Shaw, mmoja wa waandishi bora wa Uingereza. Nataka kutazama iendeleavyo na serikali yake ya kujitawala wenyewe. Hapana shaka imo katika hali ya furaha sasa.

Uingereza ni nchi ya viwanda na majahabu makubwa. Katika viwanda nataka kuona kazi mbalimbali na katika majahabu jinsi vyombo viundwavyo.

Zaidi kuliko yote nawaajabia sana Waingereza na serikali yao ya watu waliochaguliwa na watu wenyewe. Nataka kukaa kati yao ili nione furaha za maisha yao. Natamani fununu ya hekima yao ya maisha.

Kwa sababu hizi zote Uingereza ina ushawashi mkubwa nami ningependa kabisa kuizuru.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 89 - 90
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×