Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-zpzq9 Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T10:06:22.676Z Has data issue: false hasContentIssue false

27 - Maskani Bora

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Maskani, maskani mazuri

  • 2. Lazima yawe na nafasi ya kutosha

  • 3. Lazima yawe na hewa, furaha na amani

  • 4. Lazima yawe na raha zote za maisha

  • 5. Mahali pa starehe baada ya kazi ngumu ya mchana

  • 6. Lazima yasijae tele watu

  • 7. Tabia ya mapenzi, kusaidiana na ukunjufu

Kadiri yalivyo duni, hapana mahali kama maskani yetu. Tukiwa mbali na nchi yetu, mioyo yetu hulilia maskani yetu. Baada ya maisha ya ujasiri, furaha au kazi katika nchi ya mbali, roho zetu hutamani maskani yetu, haidhuru yakiwa mabaya, duni au mazuri. Kweli ni kwamba neno hili maskani lina haiba iondoayo mashaka na wasiwasi wote mioyoni mwetu. Kama maskani duni ya kawaida huweza kufanya mengi kama hayo, maskani bora huweza kufanya mengi mno kuliko hayo.

Heri tutazame twakusudia kusema nini juu ya maskani bora. Maskani bora si lazima kuwa kama Beti El Ajaib, yaliyopambwa kwa anasa au yaliyozungukwa na bustani nzuri. Maskani bora huweza kuwa hata nyumba ndogo yenye pambo la kufaa ndani yake. Katika maskani bora lazima pawe na nafasi ya kukaa. Fikiri hali ya jamaa wengi wakisongana pamoja katika nafasi ndogo nyumbani. Hasa nafasi hiyo hiyo ikilazimu kutumika kwa jiko, sebule, chumba cha kulala, chumba cha kusomea, msalani na kadha wa kadha wakati wote. Hapana hata nafasi ya kutosha watu wanne kulala vema. Lazima tuwe na chumba cha kulala, sebule ya kuketi, jiko na msalani. Lazima yawe na pambo la kupumbaza maisha pia. Lazima yawe na hewa, mwangaza mzuri na faraja.

Amani na faraja huungana na maskani. Twenda huko jioni tumechoka tena taabani baada ya kazi ngumu kwa matumaini ya kustarehesha viungo vyetu vilivyochoka tukapate amani na raha. Mahali pakiwa na kelele, hapana raha wala buraha. Tukifunga milango yetu tukaketi pamoja wote kwa muda wa saa chache kila siku, twafaidi maisha na faragha. Kwa bahati mbaya nyumba kama zile zipangishwazo mijini hazina nafasi ya kutosha kwa mambo kama haya.

Katika maskani bora lazima tupate raha zote za maisha. Tuwe na watumishi kwa kazi za nyumbani, tukiweza kuwaajiri. Lakini watu wasijae tele. Jamaa ya Mwafrika imezoea kuwa kundi kubwa. Mke, watoto, wajukuu, wazee, wajomba, mashangazi na wengine katika nyumba moja isiyo nafasi. Haya si maskani bora hata kidogo. Amani na furaha itapatikana wapi katika umati kama huu?

Hapana haja ya kusema kwamba maskani bora lazima yawe safi na nadhifu. Mtu hawezi kupata faraja wala starehe katika nyumba chafu na mbaya.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 53 - 54
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×