1. Maonyesho mbalimbali ya mapenzi
2. Maongozi ya mama juu ya tabia ya mtoto
3. Mama asiyeelimika huharibu mtoto
4. Mapenzi ya mama ni ya kujitolea, hayana choyo
5. Maneno ya mapenzi yawe na busara
Penzi la kujitolea
Ndilo penzi la daima,
Twapata kwa kuzaliwa
Na atupaye ni mama,
Hatupati kwa ulua
Kwa mali wala heshima.
Pana mapenzi kati ya marafiki, baina ya mume na mke, kaka na dada, baina ya kaka na kaka. Mapenzi yadumuyo kati ya mama na mtoto wake hayana choyo hata kidogo nayo yana nguvu kabisa. Hili hufahamika upesi. Mama hupenda mtoto wake, kwa sababu ni uzazi wake mwenyewe, na mtoto hulipa mapenzi yake kwa sababu mama ndiye amlishaye na amleaye. Kwa kuwa kiungo hiki cha kupendana huungwa utotoni, hudumu na upendo mwingi kabisa kwetu. Yajulikana sana kwamba mvuto ufanywao katika utoto wetu hushika kama muhuri juu ya nta.
Twaiga tuwaajabiao au tuwapendao. Mtoto huiga matendo ya mama au baba. Mama mwenye busara hutengeneza mara kwa mara maisha ya mtoto wake akamfanya mtu bora wa ulimwengu. Kwa hiyo pana methali mashuhuri kwamba mkono uleao mtoto hutawala ulimwengu. Wakati ujao wa mtoto umo mikononi mwa mama aleaye mtoto, na wakati ujao wa ulimwengu umo mikononi mwa watoto wa ulimwengu wataokua na kuwa raia wema. Mama akitoa mafundisho mazuri kwa kutia kidogo kidogo adili na tabia zote njema moyoni mwa mtoto, mtoto huyo atakuwa raia bora halisi. Faida hii si ya mtoto peke yake, lakini ni faida ya taifa vile vile, maana, taifa huwa bora pia.
Lakini kwa bahati mbaya, mama, hasa katika Afrika, hajui kusoma na hivyo kwa sababu ya mapenzi ya mtoto wake, humharibu tu. Mama mjinga hatunzi mtoto ila humwacha akatangatanga ovyo. Mtoto kama huyo hapati mapenzi ya mama yake. Mama mpuuzi husaidia uvivu na woga wa mtoto kwa kumdekeza. Huwa upande mmoja na mtoto mara kwa mara na humtetea baba amkaripiapo kwa neno fulani.
Licha ya hili, hapana kitu azizi ulimwenguni kama mapenzi ya mama. Mapenzi bora kabisa hutokana na kujitolea na kujisabilia. Alishapo au atunzapo mtoto mchana na usiku, hatazamii kulipwa kitu. Hata mtoto akiwa na kilema ampenda. Mapenzi ya mama hayafanyi tofauti baina ya mweupe na mweusi, mbaya au mzuri. Baba mwepesi kukasirika lakini paja la mama litayari siku zote kupakata kichwa kilichochoka cha mtoto wake.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.