Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-2z2hb Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:00:31.113Z Has data issue: false hasContentIssue false

29 - Maisha Ya Mti

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Nasaba bora

  • 2. Ushirikina na kuabudiwa na watu

  • 3. Mazungumzo ya dini chini yangu

  • 4. Tamasha karibu yangu

  • 5. Maangamizi na uzee wa huzuni

Nilizaliwa na nasaba bora. Mbingu ni baba yangu na Ardhi ni mama yangu. Tangu utotoni mchana nimevaa nuru na usiku nimejifunika giza. Kinyume cha viumbe wengine, nala kwa miguu badala ya kinywa. Hii ndiyo desturi yetu sisi miti. Kinywa hutumika kwa kusema tu kama kifanyavyo leo kwa kusimulia hadithi ya maisha yangu. Mtaona ajabu, lakini ndivyo nilivyoumbwa. Nami najivuna kama wajivunavyo viumbe wengine.

Nilianza maisha yangu miaka thelathini iliyopita. Huu si umri mkubwa kwa mti. Lakini ni mkubwa wa kutosha mkisikia mambo yaliyonipata. Nilipokuwa na umri wa miaka mitano mvua haikupatikana, Watu walianza kudhikika, nami nikakaribia kufa.

Umri wangu ulipokuwa miaka kumi palitokea dhoruba kali sana. Miti iling’oka, na nyumba kadha wa kadha zikaharibika. Mimi peke yangu ndiye niliyejizuia kwa nguvu zangu zote. Kusema kinaganaga, niliokoka kufa tu, si majeraha. Tawi langu moja lilivunjika nikaona uchungu mwingi sana. Wakati tawi lilipokuwa likianguka, lilipiga nyati aliyekuwa chini ya kivuli changu, watu wakapata nyama ya kula. Tukio hili liliamsha ushirikina wa watu tangu siku ile. Mtu mmoja aliyezoea kuabudu mizimu, alianza kuniabudu maana mti aliokuwa akiabudu kwanza ulikuwa umekwishang’oka.

Kwa kumfuata mtu huyu, watu wengine walianza kuniabudu vile vile, sijui kwa nini. Mwaka uliofuata matukio hayo mvua nyingi ilinyesha watu wakafurahi sana. Baadhi yao waliamini kwamba mvua ile ililetwa na ibada yangu nikafanywa mzimu mkubwa. Katika mwaka wangu wa kumi na tano palikuja hatibu mkubwa sana mjini kivuli changu kikachaguliwa kuwa mahali pa mazungumzo ya dini. Watu wa pande zote walikuja nikawa mahali pa haji kama Yeruselemi na Makka.

Tamasha kubwa za dini zilifanywa chini yangu nikawa katika utukufu kwa muda wa miaka kumi na mitano mfululizo. Kisha mambo yaligeuka. Siku moja watoto walikuwa wakicheza bui katika mti uliokuwa karibu na mimi. Walikuja kwangu wakaanza kucheza mchezo huo huo katika matawi yangu. Watoto kumi walisimama juu ya tawi moja. Tawi lilivunjika kwa sababu ya uzito wao; watoto wawili katika hao wakafa. Watu walichukizwa na tukio hili lakini waliendelea kuniabudu. Palikuwa na shida ya mvua katika mwaka huo huo. Na baya kuliko yote, ilikuwa ni ajali ile iliyotokea kwa watoto wale wawili. Tangu siku ile watu walinituhumu kwamba mashetani waovu walikuwa katika shina langu.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 57 - 58
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×