Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-4ks9w Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T06:39:40.261Z Has data issue: false hasContentIssue false

26 - Uthabiti Wa Mwili Na Uthabiti Wa Moyo

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Tofauti

  • 2. Mifano

  • 3. Faida za uthabiti wa mwili

  • 4. Faida za uthabiti wa moyo

  • 5. Mlingano na kinyume

Uthabiti ni adili ya kwanza ijengayo tabia ya mtu. Pana uthabiti namna mbili: wa mwili na wa moyo. Uthabiti wa mwili ni uthabiti wa kiwiliwili. Uthabiti wa moyo ni uthabiti wa dhati. Mtu mwenye uthabiti wa mwili hahofu hatari yoyote ya kiwiliwili. Mtu mwenye uthabiti wa moyo hahofu kauli ya watu.

Askari huenda vitani akapigana kwa ushujaa. Ana uthabiti wa mwili. Mchunga asiyehofu wanyama mwitu, ana uthabiti wa mwili. Mtu atanguaye ndoa ya siri wakati watu wengi wanapoipendelea, ana uthabiti wa moyo japo hutokea akawa katika upande usiofaa. Yahitajiwayo kwake ni kwamba lazima aseme au atende kama asadikivyo hasa tu.

Yasemekana kwamba waoga hufa mara nyingi kabla ya mauti yao. Hivyo uthabiti wa mwili hufaa katika mambo mengi ya maisha. Katika kijiji, mkulima yampasa kuamka usiku katika shamba lake, na mchunga yampasa kuzuru mapori mapya. Mtu hawezi kukaa kijijini bila kuwa na uthabiti wa mwili. Lakini hata mtu wa mjini hasalimiki na hatari ya watu wajiitao vikopo. Hivyo uthabiti wa mwili ni jambo la lazima. Katika nyakati za vita, si askari tu, lakini hata watu wa mji lazima wawe na uthabiti wa mwili pia. Watu wote lazima wawe tayari kwenda jeshini au kukabili shambulio la mzinga. Wanaume ni wawili, arukiwaye na arukiaye.

Uthabiti wa moyo ni kitu azizi katika adili, maendeleo ya watu au nchi. Kweli katika usemi, fikira na tendo peke yake huongoza katika maendeleo, na uthabiti wa moyo ni sehemu ya pili ya kweli. Watu wote wakipotea, lazima pawe na mmoja aliye thabiti wa kutosha kufumbua macho yao. Mambo yapasayo watu yaweza kutengenezwa watengenezaji wakiwaambia watu kweli tupu. Waongozi wa nchi wajibu wao kutanabahisha serikali ipoteapo. Serikali ikishauriwa na raia ndipo maendeleo yafanyikapo.

Hujadilika kwamba mtu, mwenye uthabiti wa mwili, ana uthabiti wa moyo vile vile. Lakini hapana haja ya kuwa hivyo. Askari atakabili kwa ushujaa risasi za maadui, lakini hawezi kuthubutu kukasiri jinsi yake. Kwa kinyume, mtetezi aweza kuleta mabadiliko makubwa katika serikali, ingawa hana uthabiti wa mwili wa kukabili simba angurumaye. Ni vigumu kulinganisha mambo haya mawili. Lakini kwa kutazama faida nyingi ziletwazo na uthabiti wa moyo kwa watu wote, ningestahabu uthabiti wa moyo kuliko uthabiti wa mwili. Ustaarabu wetu hautaki tupigane na simba au chui, lakini watutazamia kuongoza watu na nchi katika usitawi kwa uthabiti wetu wa moyo.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 51 - 52
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×