Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-gmt7q Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:43:03.769Z Has data issue: false hasContentIssue false

21 - Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Ni methali maarufu sana

  • 2. Matumizi yake kwa mambo mbalimbali ya maisha

  • 3. Yaonya utaratibu wa kazi

  • 4. Tabia mbaya zikomeshwe mwanzoni

  • 5. Tusidharau madogo

  • 6. Lazima tujiandae mapema

Methali hii nyepesi lakini maarufu sana. Mamoja kwa sababu ya wepesi wake, tusiidharau.

Ni jambo lijulikanalo na watu wote kwamba ukuta wa nyumba upasukapo, lazima tuuzibe upesi. Tusipofanya hivyo mapema ufa utazidi nao utahitaji kazi kubwa ya kuutengeneza. Pengine ukuta huweza kufanya ufa mkubwa sana, hata ni vigumu sana kuutengeneza. Kweli iliyo juu ya ukuta ni kweli juu ya nguo, viatu, magunia, madaraja, meli na vingine. Dosari ndogo katika vitu kama hivi lazima zitengenezwe mapema.

Methali hii huweza kutumiwa kwa mambo mbalimbali ya maisha. Mtu akipatwa na ugonjwa, asiudharau, lakini amshauri upesi mganga. Hili litamwepusha na maumivu mengi ya wakati ujao na uharibifu wa fedha. Akidharau, ugonjwa waweza kuwa hauponyeki ukamtia katika mauti.

Dosari ndogo katika eropleni, mashine kubwa na magudi lazima zitengenezwe mapema, kama sivyo hazitatengenezeka.

Methali hii husema lazima tufanye kazi yetu kwa kawaida. Mwanafunzi akisoma masomo yake kwa kawaida, hufaulu kwa urahisi. Lakini akiacha masomo yake akajikalia bure, atajiona amezongwa na mashaka makubwa ya masomo. Yamkini hata kwa bidii zake, ataona shida kufanikiwa.

Tabia mbaya lazima zikomeshwe mwanzoni vile vile. Wazazi au walimu wakiona watoto wadogo wavivu au fedhuli, lazima wakanywe. Wizi wa kalamu au mpira wa kufutia ni neno dogo. Lakini lazima lizuiwe mapema. Kama sivyo mtoto aweza kuwa mwizi mkubwa. Watu wengi hunywa ulevi ili kujiburudisha, lakini ulevi huwalafua mara moja wakawa walevi wakubwa. Kwa hivyo tabia mbaya kama hizo lazima zikomeshwe mwanzoni.

Twaonywa na methali hii kwamba tusidharau madogo. Pengine madogo huwa makubwa yakazaa matata mengi. Imesemwa kweli kwamba “Ufa huzamisha merikebu.”

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 43 - 45
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×