Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-xlmdk Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:10:16.646Z Has data issue: false hasContentIssue false

25 - Ubora Wa Madogo

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Kwa desturi madogo hudharauliwa na watu

  • 2. Matokeo yake mabaya

  • 3. Ni mafundisho ya mambo makubwa katika maisha

  • 4. Thamani na ubora wa madogo

“Gome huziba gogo, mti humea kwa chane,

Madogo yana vurugo, watu wasitambuane!”

Kwa desturi madogo hudharauliwa kwamba si kitu wala hayana maana, lakini tukitulia kufikiri matokeo yake tusingeyaona kama hivyo. Twahesabu vitu vingi kwa ukubwa wake na kwa hiyo tundu ndogo katika nguo zetu, au jipu au mkata mdogo katika miili yetu, hudharauliwa mwanzoni mpaka ulete hatari na matokeo mabaya. Jipu au mkata mdogo kidoleni hudharauliwa, lakini huoza ukaeneza sumu katika mwili mzima. Pengine sehemu ya mwili hupasa kukatwa, au hata mauti hutokea. Hali kadhalika katika mambo yetu ya fedha na gharama twadharau sarafu ndogo, lakini methali hutuonya, “Haba na haba hujaza kibaba.” Mifano isiyohesabika huweza kuonekana katika maisha ionyeshayo hasa kwamba madogo huwa makubwa kabisa. Skrubu moja ni kitu kidogo katika mashine kubwa ya eropleni, lakini eropleni zimeangamia, kwa sababu skrubu haikufungwa barabara. Katika maongezi yetu wenyewe hatufikiri vile vile maneno ya ovyo na uzembe tusemayo juu ya watu wengine, lakini pengine huzua taksiri na uchungu.

Vyango na misumari ni vitu vidogo, lakini huunganisha majengo, meli, na madaraja makubwa kabisa. Kipande cha sigara au kijiti cha kibiriti chenye moto ni kitu kidogo, lakini huwa mara kwa mara sababu ya moto wa maangamizi makubwa. Neno ni dogo lakini laweza kumimina asali au kufuma mafumo mioyoni mwa wengine. Ufa au tundu ndogo melini huweza kuwa si kitu, lakini huweza kuzamisha meli nzima. Vita katika maisha hushindwa kwa madogo na hupotea kwa madogo.

Katika maisha vile vile, neno laweza kutupatia rafiki au adui. Laweza kuzua ugomvi au uchungu nyumbani likaharibu amani na furaha. Asili ya maisha ni mambo madogo.

Tukijali madogo, uwezo wetu wa kuangalia huzidi kuwa mzuri. Twapata akili tambuzi na ndimi zetu hujifunza kutii na kujitawala. Kuzingatia sana mambo madogo katika maisha kwafundisha akili. Kama hatujui kutumia madogo, hatuwezi kujifunza namna ya kujaribu mambo makubwa katika maisha. Mtu aliye mwangalifu katika mambo madogo huwa mwangalifu katika makubwa. Mtu awezaye kuona dogo hawezi kushindwa kuona mambo makubwa, kama mtu, ambaye ana macho makali ya kutosha kuona sindano, hawezi kushindwa kuona mlima. Lakini madogo yakidharauliwa au yasipohesabiwa kabisa, kisasi yakatuangamiza.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 49 - 51
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×