Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-7l9ct Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T06:34:33.466Z Has data issue: false hasContentIssue false

32 - Ubora Wa Ibada

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Ibada zina auni kubwa

  • 2. Kila dini imekubali ubora wake

  • 3. Ibada za watu mbalimbali

  • 4. Faida za ibada

  • 5. Matokeo ya ibada

  • 6. Mifano

  • 7. Hadhari katika ibada

Ibada zina auni kubwa katika maisha. Mambo mengi hufanyika kwa ibada katika dunia hii.

Kila dini imekubali ubora wa ibada. Ukristo, Islamu na nyingine zimesisitiza sana ibada kwa sababu zafaa sana.

Ubora wa ibada hutegemea juu ya mtu aabuduye. Katika ibada zote, zile za watoto ni safi kabisa. Zafanana na harufu takatifu ya ubani na hupata kabuli ya kwanza kwa Mungu. Ibada za wanawake zina mvuto na hutoka katikati ya keto za mioyo yao. Ibada za wanaume wengi zina choyo na haraka. Hivyo hazina nguvu.

Faida za ibada ni nyingi, ingawa wingi wa faida zenyewe hauonekani kwa macho. Hubariki watu waabuduo tena hutakasa mioyo na akili zao. Fikira zao huwa bora. Hutukuzwa hapa duniani mpaka peponi. Hupata ridhaa na amani ya moyo. Wale waabuduo kila kipindi huwa wema, karimu na watawa. Hutenda mambo mema wakasaidia wengine siku zote. Ibada huwapa nguvu ya kuvumilia maumivu na taabu tena, huwaongoza kwa Mungu.

Matokeo ya ibada yana ajabu kubwa sana. Yana nguvu nyingi mno kuliko silaha zote zikiwekwa pamoja, nayo yanakwenda upesi mno kuliko fataki. Huvuka bahari yakashinda na malimwengu. Hufanya miujiza ambayo ujuzi hauwezi kuieleza. Sisi sote twajua kwamba ibada hugeuza kushindwa kukawa kushinda, nazo huweza kufukuza wajumbe wa mauti kando ya mtu anayekufa. Zina nguvu nyingi sana hata hugeuza mioyo ya waovu kabisa wakawa wema. Ibada nyingi sana hufanywa kwa sababu ya kutaka msaada wa Mungu. Kwa hiyo twawaombea maisha marefu watu wakubwa, twaombea amani roho za wafu, twaomba kupata mvua, na matokeo yake hufurahisha kabisa. Dua likikubaliwa na Mungu, majibu hushuka mbinguni kama umeme.

Ubora wa ibada umeonyeshwa maridhawa katika hadithi nyingi. George wa V alipoomba katika Vita Kuu ya Kwanza alishinda majeshi ya Kaizari, Katika Vita Kuu ya Pili, George wa VI aliomba akashinda majeshi ya Nazi.

Lakini tukitaka kuimarisha ibada, lazima tuabudu kwa moyo mweupe. Pasiwe na malalamiko wala choyo katika ibada zetu. Kwa hivi mtu asiombe kupata mali na furaha zake mwenyewe. Tena tukiabudu kwa muda wa dakika chache na tukiwinda kutwa watu wengine, Mungu shida kutusaidia.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 62 - 63
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×