Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-4ks9w Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:06:05.855Z Has data issue: false hasContentIssue false

48 - Mazoezi Ya Mwili

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Uhusiano baina ya mwili na akili

  • 2. Sababu ya uharibifu wa mwili

  • 3. Dawa ni mazoezi ya mwili na mchezo

  • 4. Mazoezi ya mwili ndiyo mwongozo peke yake

  • 5. Faida za mazoezi ya mwili

Kuna methali isemayo, “Akili razini ni afya mwilini.” Twaambiwa waziwazi na methali hii kwamba lazima tuwe na mazoezi ya mwili na mchezo, nasi twaonywa kwamba tusitupe mwili ukaharibika kwa sababu ya kusitawisha akili. Twaweza kuwa na akili razini kama tuna mwili wa afya tu.

Kwa desturi watu wote huzaliwa na mwili wa afya, lakini baadaye kwa sababu ya desturi mbaya au kwa sababu ya ukosefu wa sulubu ya kiwiliwili, mwili huanza kuharibika. Ni dhahiri kwamba kitu kisipotumiwa, huoza. Kukomesha uharibifu huu, mwili lazima uzoezwe kila siku katika namna fulani ya sulubu ya mwili. Njia bora ni kwamba kazi zetu lazima ziwe na sulubu ya mwili, kama tuonavyo katika maisha ya mkulima, mhunzi au hamali.

Kwa sababu hii twaona kwamba mazoezi ya mwili yametiliwa mkazo mwingi sana katika idara zetu za elimu. Kusoma si kazi nyepesi. Hakutumii akili tu lakini mwili hutumiwa vile vile. Kama vyuo havisisitizi mazoezi ya mwili hapana shaka wanafunzi wake watakonda na kuwa magofu. Wanafunzi wengi wangeonekana wamezeeka kabla ya wakati wao. Wangekuwa na sura za kusawajika na miili dhaifu. Ni jambo la maana sana kulazimisha mazoezi ya mwili katika vyuo, kwa sababu wakati wa ujana ndiyo wakati wa kuweka msingi wa afya mwilini. Hakika kubwa ya jambo hili inapatikana katika methali nyingine maarufu isemayo kwamba “udongo upate ungali maji”.

Haikaidiki kwamba mazoezi ya mwili ya lazima huchukiza kwa wanafunzi mwanzoni. Husemwa kwamba nusu saa ya kuchezesha mikono na miguu nje haina manufaa kwa mtu yeyote, kwamba hufaa kwa onyesho na kwamba ni kupoteza wakati bure. Lakini fikira kidogo huonyesha kwamba ina manufaa mengi sana. Ingawa nusu saa ya mara moja au mara mbili kwa juma moja haileti faida papo kwa papo kwa mwanafunzi, lakini hufumbua macho yake aone faida za mazoezi ya mwili. Mazoezi ya mwili ni mwongozo na onyo kama mafundisho mengine yafundishwayo katika vyuo vya elimu.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 90 - 92
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×