Published online by Cambridge University Press: 17 April 2025
1. Maongozi bora ya mama bora
2. Maongozi yake katika utoto
3. Maongozi yake baadaye
4. Mama hulinganishwa na walimu wa ulimwengu
5. Maongozi ya mama mbaya
6. Maongozi ya milele ya mama mwema
Mtoto huongozwa sana na mama yake. Mama mmoja mwema sawa na walimu wote wa ulimwengu. Nyumbani huwa kama sumaku katika mioyo ya wote, na nyota ya mwongozo katika macho ya wote.
Maongozi ya mama huanza siku ya kuzaliwa mtoto. Hawezi kujizuia kuiga aonayo. Kila neno kwake huwa mfano na mfano bora ni mama yake. Kumwiga kwake hakubadiliki. Mtoto hujifunza kwa mfano wa mama yake, akajitengeneza kwa kuiga desturi, usemi na tabia yake.
Mama mwema ni mwalimu wa kwanza naye ndiye mwenye mvuto mwingi kabisa kwa mtoto wake. Mfano mwema awekao mbele ya mtoto wake hutokea katika wakati ujao, ukaleta faida. Maskani yenye mama mwema ni skuli bora kabisa. Huko mtoto hujifunza masomo ya ukunjufu, saburi, kujitawala na maana ya kazi na utii. Mama mwema hufundisha somo la adabu vile vile. Hivyo kabla va mtoto kwenda skuli, amejifunza mambo mengi ambayo walimu wasingaliweza kuyafundisha.
Hata mtoto aendapo skuli, maongozi ya mama hudumu. Humwadilisha mtoto akampa mawazo safi na mema. Humfundisha kuwa mwangalifu na mwadilifu katika masomo yake wala hamruhusu kwenda na watu wabaya. Mwalimu wa skuli afundisha masomo kwa vitabu, lakini mama mwema afundisha kila neno lifaalo kwa maisha. Mwalimu wa skuli humpasa kufundisha watoto wengi, lakini mama yampasa kufundisha watoto wake mwenyewe tu. Basi si ajabu kwamba afanya kazi ya walimu wote wa ulimwengu.
Zaidi ya walimu wa skuli, pana mahakimu. Mahakimu hufundisha kwa sheria. Hawa si walimu wabaya. Kazi yao kubwa ni kufasiri sheria. Wacheka, lakini kama ujuavyo, sheria ni upanga wa makali pande zote. Hukata huku na huko. Mafundisho yake yana gharama kubwa, uchungu mwingi na hupoteza jina la mtu mara kwa mara.
Lakini mama akiwa mbaya, huwa mbaya mno kuliko mwalimu mbaya na sheria kali kabisa. Weka mtoto katika ulinzi wa mama mpuuzi, mjinga, na hapana elimu wala sheria baadaye itayoweza kuondoa uovu aliotenda. Mama akiwa mvivu na mwovu, watoto wake watavia tena watapotoka vibaya sana.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.