1. Amri ya Agano Jipya
2. Fundisho la Islamu
3. Wajibu wetu kwa majirani zetu
4. Sababu za uharabu katika akraba zetu kwa majirani
Amri moja katika amri kumi za Agano Jipya ni “Mpende jirani yako.” Hustaajabisha kwa nini Ukristo umetia mkazo mwingi sana juu ya tabia yetu kwa majirani zetu lakini msahafu huu huu hausemi neno juu ya kupenda mke au mtoto! Tungeingia ndani kidogo, tungefahamu mara moja kwamba twapenda watoto na wake wetu bila mtu yeyote kutuamrisha kuwapenda. Lakini yafaa kabisa tuonywe lipasalo kutenda kwa majirani zetu. Kwa hivi Agano Jipya lasema kwamba tabia yetu kwa majirani zetu lazima iwe ya mapenzi.
Kwa maneno mawili, “Halahala jirani,” Islamu hukariri fundisho hili hili. Ujirani katika Islamu haukomi nyumba ya pili wala ya tatu tu, lakini mpaka nyumba arobaini zilizo pamoja. Kwa hiyo mawazo ya Wakristo na Waislamu ya tabia juu ya jirani ni mamoja kabisa. Kwa kuwa majirani hukaa pamoja, akraba kati yao huzidi nguvu nao hujuana zaidi, hivyo baadaye huishi kama watu wa ukoo mmoja. Majirani Waafrika katika muda mdogo huweza kula na kunywa pamoja, jambo ambalo nadra kupatikana kwa makabila mengine.
Kuna kazi fulani mtu atazamiwazo kumtendea jirani yake. Lazima asaidie jirani yake katika nyakati za ugonjwa, ajali au hatari. Mume akiwa hayupo, lazima atazame salama ya nyumba na watoto wake. Katika shida zote, jirani awe tayari kusaidia siku zote. Lazima atazame vile vile kwamba kwa hali yoyote asijifanye udhia kwa jirani yake. Ni wajibu wake asifuje usingizi na amani ya majirani zake wakati wanapopumzika. Kuna watu wawezao kupiga santuri au kufungua idhaa zao bila kujali hata kidogo faraja ya majirani zao. Hawa hukirihi sana wenzao. Majirani haifai kugombana. Mabibi waangalie sana onyo hili, maana, wanawake wana mazoea mabaya ya kukimbilia kugombana na mke wa jirani kwa neno dogo kabisa.
Kwa sababu ya mabadiliko katika hali za maisha ya watu, pana upungufu wa akraba baina ya majirani. Sababu yake ni kwamba wengi katika sisi tumeacha vijiji vyetu nasi tumekaa mijini. Tabia ya wengi katika miji ni kujifungia nyumbani mwetu tukakutana na majirani zetu wa nyumba ya pili kwa bahati tu. Hili halipatikani vijijini ambako kila jioni majirani hukutana wakaongea pamoja vema sana.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.