Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-px5tt Total loading time: 0 Render date: 2025-05-10T04:44:09.086Z Has data issue: false hasContentIssue false

42 - Kusudi Langu Katika Maisha

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Kusudi langu kubwa

  • 2. Nachagua uandishi nipate kusudi langu

  • 3. Mashaka ya uandishi na saburi

  • 4. Kunyonya maarifa kwa matiti badala ya chupa

Kila mtu duniani, kadiri alivyo mdogo au mkubwa, ana kusudi lake katika maisha. Mwana wa mfalme aweza kuwa na kusudi la kuwa mfalme, na mfalme aweza kuwa na kusudi la kuwa mfalme mkuu. Jemadari akusudia kuwa amirijeshi, na askari akusudia kuwa jemadari. Kusudi la fulani ni kupata sifa, fulani kupata uwezo, fulani kupata utajiri na fulani kutaka elimu.

Mambo yakiwa hivi, hata mimi nina kusudi langu katika maisha, ingawa sijui nitajaliwa kulipata lini. Sitaki kutafuta fedha, wala heshima au umaarufu upatikanao bila shida. Kusudi langu katika maisha ni kujipatia mimi mwenyewe na wenzangu furaha. Kupata kusudi hili nimeazimu kuwa mwandishi na kutumia maisha yangu katika kusaidia wasomaji. Naamini kwamba nimefanya uchaguzi mwema. Nikiwa Mwandishi wa maana, nitapata fedha ambayo nitatumia kwa kufadhili maskini. Sitaandika kazi hafifu; na bora nitazojaliwa kuandika sitauza kwa thamani kubwa. Kazi zangu zitakuwa bora lakini rahisi kununulika ili zisaidie jitihadi ya kupigana na ujinga. Nikijaliwa kuwa mwandishi hodari, hapana shaka nitapata sifa na umaarufu, kwa sababu nitazungumza na ulimwengu badala ya watu wachache. Lakini nitajihadhari nisighurishwe na kiburi kwa sababu ya sifa hii. Uandishi ni kazi ya unyenyekevu. Haja niliyo nayo ni kusema fikira zangu na kuacha wasomaji waamue. Sitakuwa mwamuzi wa kazi zangu. Nikifunguliwa heri na kazi zangu zikienea kila pembe, neno gumu kupatikana ingawa nalitamani, hapana budi nitapata uwezo na maongozi. Lakini nitajihadhari nisiharibu uwezo wangu kwa kuandika kazi yoyote ya aibu au isiyostahili. Kwa ufupi, nimekusudia sana kuwa mwandishi, si kwa sababu ni kazi ambayo itaniletea utajiri, sifa au uwezo mkubwa mno kuliko kazi nyingine yoyote, ila kwa sababu ina nafasi bora na kubwa sana za kutumikia watu katika pigano la kila siku la elimu na ujinga.

Mwandishi akipanda mbegu yake mara moja hapana kiangazi kiwezacho kukausha wala masika yawezayo kutotesha mmea wake. Kwa mtu mnyonge kama mimi, kazi gani nyingine bora kuliko hii? Ila za uandishi ni kwamba hauna mazao ya haraka. Mashaka mengi yatapasa kuvumiliwa. Naweza kuishi nikafa bila kuona mavuno yake lakini pana hakika ya kupatikana nipo au sipo duniani. Naomba nijaliwe saburi ya manabii wakati kazi zangu zikikataliwa lakini nisiache kusudi langu.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 80 - 81
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×