1. Watoto ni katili kwa wanyama
2. Watu wazima ni katili pia
3. Wanyama ni wasaidizi wetu
4. Wanyama mabubu wasitendewe ukatili
5. Sheria juu ya ukatili
6. Huruma haigharimu kitu
Wanyama wana maono kama watu. Waona maumivu kama sisi tuonavyo. Mchomo wa sindano una maumivu kwa wanyama kama kwetu sisi. Kwa hivyo hutupasa kuhurumia wanyama.
Watoto ni katili kwa wanyama mara kwa mara. Mtoto huweza kukokota paka au mbwa kwa takua. Pengine mtoto hutupia vyura mawe katika kisima, na pengine hupiga mbuzi au ng’ombe kwa fimbo. Hata punda na farasi hawana salama kwa watoto watukutu. Bila shaka, wafanya hivyo kwa mchezo, lakini mchezo wao ni maumivu ya wanyama mabubu. Kwa hivyo lazima watoto wafundishwe kuhurumia wanyama.
Hata watu wazima ni katili kwa wanyama. Ng’ombe, farasi nyumbu na punda hutendewa ukatili na watu. Pengine hulemezwa mizigo mizito wakalishwa chakula kidogo. Hata wakiwa wagonjwa hulazimishwa kufanya kazi. Kama kwamba hili halitoshi, hupigwa bila huruma. Mara kwa mara ndama hufishwa kwa njaa ili watu wapate maziwa mengi kwa ng’ombe. Ukatili wa watu wazima huchukiza mno kuliko ule wa watoto.
Wanyama ni wasaidizi wa wanadamu. Watusaidia katika kazi mbalimbali kama uchukuzi na kulima. Vinyesi vyao ni mbolea ya rutuba kabisa katika makonde yetu. Nchi yenye wanyama ina akiba kubwa ya chakula, manyoya, pembe na ngozi.
Ukatili kwa wanyama mbaya mno kuliko ukatili kwa wanadamu, maana watu waweza kutaradhia, lakini wanyama hawawezi. Wanyama ni mabubu, viumbe wasio msaada wala hawawezi kujitetea. Tajiri akidhulumu mtumishi wake, mtumishi aweza kuacha kazi akaenda pahali pengine, lakini mnyama mnyonge hawezi kufanya neno. Mtumishi akiugua, aweza kukataa kufanya kazi, lakini mnyama bubu hana maneno ya kutetea haki yake. Yampasa kufanya kazi ngumu katika hali ya kuhuzunisha kama hiyo. Ukimpiga mtumishi sana, aweza kwenda katika baraza ya sheria, lakini ng’ombe au mbuzi wako hawezi kukufanyia mashtaka yoyote. Kwa hivyo ni wajibu wa kila mwanadamu kuhurumia wanyama.
Siku hizi serikali za nchi nyingi zimeamrisha sheria juu ya ukatili wa wanyama. Mtu yeyote aonekanaye anatenda ukatili kwa mnyama huadhibiwa na baraza ya sheria. Tena kuna vyama vya kuzuia ukatili kwa wanyama mijini viokoavyo wanyama katika ukatili. Vyama hivyo husaidia vile vile katika utabibu wa wanyama.
Huruma ni adili kubwa nayo haigharimu kitu. Basi kwa nini tuwe mabahili katika kuhurumia wanyama? Mungu hupendezwa mno na matendo yetu mema kwa wanyama kuliko na ibada zetu.
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.